Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) ni chama cha Siasa kilichopata usajili wake wa kudumu tarehe 05 Mei, 2014. Chama hiki kimeundwa kupigania uwajibikaji, uadilifu, haki na uwazi katika uendeshaji wa Serikali kikiamini kuwa hiyo ndio njia ya kweli ya kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.
ACT Wazalendo kinaamini katika Demokrasia na Uhuru wa mawazo na matendo. Uzalendo kwa nchi ni miongoni mwa nguzo kuu zinazoongoza chama hiki. ACT Wazalendo ni jukwaa huru kwa kila mtanzania anayeonewa na kukandamizwa. Karibuni tupiganie nchi yetu na maslahi yetu kama watu huru.
MISINGI YETU
- Uzalendo
- Usawa
- Kupinga na Kupiga Vita Ubaguzi
- Uadilifu
- Uwazi
- Uwajibikaji
- Demokrasia
- Uhuru wa Mawazo na Matendo
- Utu
- Umoja
Kujenga Taifa la Wote, lenye ustawi, ambalo kila raia anapata maslahi yake.
Kuhakikisha utajiri wa nchi unatumika kuimarisha zaidi maisha ya watu na kuchochea uwezo wao katika kuchangia na kujenga uchumi shirikishi ambapo kila mtu ana fursa sawa za maendeleo.
Viongozi Wetu

Omar Said Shaaban
Mshauri Mkuu wa Sheria na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar
Omary Ali Shehe
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
Ester Akoth Thomas
Naibu Katibu Mkuu
Ado Shaibu Ado
Katibu Mkuu
Ismael Jussa Ladhu
Makamu Mwenyekiti Zanzibar
Isihaka Rashid Mchinjita
Waziri Mkuu Kivuli
Othman Masoud Othman
Mwenyekiti wa Chama
Dorothy Jonas Semu
Kiongozi wa ChamaViongozi Wastafu

Juma Duni Haji
Mwenyekiti wa Chama Mstaafu
Maalim Seif Sharifu Hamad
Mwenyekiti wa Pili wa Chama Mstaafu